1. Fanya utafiti wa kutosha kuhusu shirika,Hii
itakusaidia kujibu maswali kwa wepesi.
2. Jiandae kwa maswali ya usaili wa simu,hakikisha
unayasoma maswali ya msingi katika usaili wa simu na upate majibu mapema kabla
ya usaili
3. Tumia simu ya mezani/simu ya mkononi yenye mawasliano
ya uhakika,Ili kuepuka simu kukatika wakati wa usaili.
4. Zima muito wa kusubilisha(Turn off call waiting) Hii
itaondoa usumbufu wa kupigiwa simu wakati unaongea na itakutoa katika ufanisi
wa usaili.
5. Kaa sehemu yenye utulivu,Epuka kukaa kwenye kelele ya
vitu na watu mbalimbali kama vile mashine au hata watoto wadogo
6. Uwe na gilasi ya maji,hii itakusaidia kulainisha koo
wakati unaoongea na utakunywa kwa haraka na kuendelea na mazungumzo
7. Chukua kumbukumbu, ni vema ukaandika baadhi ya mambo
ya msingi ili iwe kumbukumbu kwa baadae itakapohitajika.
8.Sikiliza kwa umakini,Ni vema ukasikiliza ili kuulewa
kile kinachoulizwa na uweze kujibu na
kama hujaelewa ni vema ukauliza ufafanuzi zaidi.Kumbuka kuchukua sekunde kadhaa
kabla ya kujibu ili kuweza kuyaweka mawazo yako pamoja kwa ufanisi,
usiharakishe kujibu.
9. Andaa maswali ya kuuliza mapema,Pale utapopewa fursa
ya kuuliza hakikisha uko tayari na maswali yako.
………..Maktaba YETU leo……….
. “Strength does not come
from winning. Your struggles develop your strengths. When you go through
hardship and decide not to surrender, that is strength”
– Arnold
Schwarzenegger
Post a Comment