Wakati wa
usaili ni wakati muhimu na hadimu sana,hivyo unahitaji umakini wa hali ya juu
zaidi katika matumizi yake.Baadhi ya maswali unaweza kuyauliza kumbe ndo
inakuwa safari yako ya kupoteza ajira.Hivyo maswali mengine ni ya kufanya
utafiti na mengine ni ya kumuuliza mwajiri mara baada ya kupata fursa
unayoomba.Yafuatayo si maswali ya kuuliza katika usaili…
1. Mtanipa mshahara kiasi gani?Swali hili si sahihi wakati
wa usaili sababu kubwa ni kwamba suala la mshahara litakuja mara baada ya
kuchaguliwa katika nafasi husika kutokana na uwezo wako katika usaili.Pia ni
vema ukafanya utafiti kuhusu mshahara mapema ili uje viwango kulingana na
nafasi unayoomba.Kumbuka mara baada ya kupata fursa ndipo mtakapojadili suala
la mshahara nawewe utaona kama kiwango kinafaa.
2.Ni lini kiwango cha mshahara wangu kitapanda?Hili
swali ni baya pengine kuliko la kwanza.Kuhusu kupanda kwa mshahara inategemea
baadhi ya mashirika yako na utaratibu wa wazi lakini mengine hayako
hivyo,jambo la msingi niwewe kufanya utafiti wa kina pindi unapopata kazi
husika.Zingatia kwamba wakati wa usaili wewe unatakiwa kuangalia suala la
kutetea nafasi uloomba sio kuchunguza maslahi.
3. Je utaratibu wa likizo ukoje katika shirika hili? Swali
hili ukiliuliza ni wazi kwamba uanonesha kuwa hujafanya utafiti wa kutosha
kuhusu shirika,lakini jambo la kuzingatia hapa ni kwamba suala la likizo mara
nyingi ni taarifa ambazo si za siri ni wajibu wako kufuatilia kwa kina kabla
hata hujaomba kazi ili upate kujua wakati mwingine huwekwa hata kwenye mtandao
wa shirika.
………..Maktaba
YETU leo……….
“Never hire someone who knows less than you do about what
he’s hired to do.”
Malcolm Forbes, Forbes
Post a Comment