Home » » Hii ndo njia rahisi ya kujibu hili swali..(What is your greatest weakness?) soma sentensi hizi

Hii ndo njia rahisi ya kujibu hili swali..(What is your greatest weakness?) soma sentensi hizi

Written By Unknown on Thursday, August 28, 2014 | 8:03 AM

            What is your greatest weakness?
Bila shaka utakubaliana na mimi kuwa swali hili si geni kabisa  katika maisha yako ya usahili na pia ni dhahiri kuwa kumekuwa na mitazamo mbalimbali ya namna ya kujibu swali hili.Siku ya leo baada ya kufanya tafiti mbalimbali na kuweka mkusanyiko kutoka kwa watalaam mbalimbali zifuatazo ni mbinu thabiti za kukaribiana na swali hili wakati wa usahili pindi utakapoitwa kwenye usahili.
1. Eleza ujuzi ambao si muhimu kwa kazi uloomba( mentioning skills that aren't critical for the job)
Mbinu mbadala ni kuchambua ujuzi muhimu na uwezo unaohitajika kwa  nafasi ulioomba na kisha eleza  kasoro ambayo si muhimu kwa ajili ya mafanikio katika kazi hiyo.mfano kama unaomba nafasi ya uuguzi ni dhahiri kwamba utatumia muda wako mwingi kuongea na mgonjwa mmoja mmoja katika kujua halia yake na kutambua namna ya kumsaidia,Hivyo jibu rahisi sana katika swali kuhusu udhaifu wako ni kwamba wewe huna uwezo mkubwa katika majadiliano ya makundi.Hiyo ni wazi kwamba unauwezo mkubwa sana wa  kuongea na mtu mmoja mmoja ambalo ndo jukumu kubwa wa muuguzi hapo utakuwa umejibu swali kwa kiwango cha juu kabisa.
2. Eleza ujuzi ulopata kulingana na uzoefu (Mention Skills You Have Improved)
Njia nyingine ni kujadili ujuzi ulopata kutoka katika kazi yako ya awali ambapo kabla yalikuwa ni madhaifu yako, hivyo  ni dhahiri kwamba utamwonesha mwajiri  kwamba unaweza kufanya maboresho  pale itapohitajika.Unaweza elezea hatua kadhaa ulizochukua katika kufanya maboresho hayo.Hii itamuonesha mwajiri wako namna utavyoweza kukua katika nafasi atakayokupa.
Kumbuka kuwa unapotumia mkakati huu epuka kutaja chochote ulichoboresha chenye uhusiano wa moja kwa moja na nafasi uliyoomba hii itakupunguzia maswali zaidi katika eneo hilo.
3. Badililisha hasi kuwa chanya(Turn a Negative into a Positive)
Unapoulizwa kuhusu madhaifu yako ni rahisi sana unaweza kubadili kilicho hasi kuwa chanya mfano,unaweza sema udhaifu wako ni kuona shughuli iliyopangwa inafanyika kwa haraka na mara nyingi unafanyakazi kwa nguvu nyingi na hata kiasi cha kukosa raha mpaka huone jambo limekamilika.
Ni dhairi kwamba hilo litamwonesha mwajiri wako kuwa inafaa na anakila sababu ya kukuajili kwa sababu utaweza kufanya kazi kwa wakati ulopangwa kwa kizungu wanasema utameet deadline.

Tazama mifano hii ambayo itakupaulewa zaidi  ya kile kilichoelezwa na bila shaka baada ya hapa hutaweza kuhofu juu ya swali hii tena na ndo maana tunasema hakuna kisichowezekana.Mifano hii ipo katika lugha ya kiingereza bila shaka utailewa kwa ukaribu

“When I'm working on a project, I don't want just to meet deadlines. Rather, I prefer to complete the project well ahead of schedule”.
“I used to wait until the last minute to set appointments for the coming week, but I realized that scheduling in advance makes much more sense.”
“I used to like to work on one project to its completion before starting on another, but I've learned to work on many projects at the same time, and I think it allows me to be more creative and effective in each one.”

“I had difficulty with calculus during college, but I persevered with tutoring assistance and extra effort and completed 2 levels with a B minus average.”
Share this article :

Post a Comment

 
Owner : Amewezaje team | Join us on Facebook | Welcome again
Copyright © 2015. Amewezaje - All Rights Reserved
Designed by Kijiwe Cha Wasomi