Utafiti wa wataalum mbalimbali unaonesha watu wengi wanaandika barua za kazi kama daraja la kumwelekeza mwajiri asome "CV" zao,kosa hili linawagharimu kila uchao kwani mwajiri asipovutiwa na barua hawezi kusoma "CV" bali huweka pembeni na kusoma za wengine.Zingatia hizi hatua tatu ili utoke katika wimbi hilo
1. Andaa barua ya kielelezo(Creat a cover letter Template)
Katika
barua hii andika taarifa zote za msingi
zinazotakiwa katika barua kama vile ujuzi pamoja na uzoefu ulonao.Kisha hifadhi
barua hiyo kwenye kompyuta yako au vinginevyo ambapo ni rahisi kuiona.
2. Binafsisha barua yako(Personalize
Your Cover Letter)
Kila
wakati utapataka kuomba kazi fungua kielelezo na tengeneza nakala nyingine kisha
anza kubadili taarifa zilizopo ili ziendane na sehemu unayotuma maombi.
· Badili anwani,ili uandike anwani ya
mwajiri unayemtumia
· Badili Cheo/salaam za awali cha/za Yule
unayemtumia,andika jina lake kama unalifahamu mfano “Dear Ms Jones” "Human Resource Manager"
· Badili aya ya kwanza,ili kueleza
nafasi unayoomba na ulipoona tangazo husika.
Badili kiini cha barua,kwa kuandika
ujuzi na uzoefu unaohitajika kulingana mchanganuo wa kazi husika
Aya yako ya mwisho pamoja na sahihi
havina haja ya kubadilishwa
· Hakikisha unahifadhi kila barua unayotuma ili kukusaidia katika
kumbukumbu
Njia hii ni rahisi sana
kuliko kuanza kuandika barua mwanzo na pengine uko na muda mfupi sana ni rahisi
kusahau mambo mengi ya msingi.Hii itakufanya kuepuka kuandika barua
isiyonamvuto inyosema “Tazama CV yangu”
3.
Hakiki barua yako kabla ya kuituma
Hii itakusaidia kubaini makosa madogo madogo kama ya herufi na
sarufi ambapo ukituma hivyo yataweza kukugharimu.
………..Maktaba YETU leo……….
Post a Comment