
Usaili
wa uso kwa uso(Face to Face Interview)
Katika aina hii ya usaili mara nyingi unaweza
kuhusisha mazungumzo kati ya mtu na mtu
.Katika usaili huu jambo la kuzingatia ni kuhakikisha unajikita kwa Yule anayekuuliza
maswali kwa kumtazama usoni,kumsikiliza na kujibu maswali pale unapoulizwa.
Lengo kuu kwako ni kuonesha uwezo wako kwa mwajiri
na uoneshe ni vipi unaweza kuleta manufaa kwa shirika au taasisi husika.
Usaili wa jopo(Panel Interview)
Katika usaili huu kunakuwa na mtu zaidi ya moja
mara nyingi watatu hadi kumi.Huu ndo wakati wako mzuri wa kuonesha uwezo wako
wa kuongoza na kuwasilisha katika kwa kundi linalokufanyia usaili.
Kwa kipindi kifupi jitahidi kuhakikisha unasoma na
kutambua tabia za kila mmoja na jitahidi kutafuta namna ya kuendana na tabia ya
kila mmoja.
Kumbuka kuchukua muda na kuwa makini katika kujibu maswali.Jitahidi kuwatazama
wanajopo pale unapoulizwa swali na
kumtazama anayekuuliza swali.Zingatia matumizi ya lugha ya mwili muda wote
unapofafanua hoja.
Endelea kufuatilia aina nyingine za usaili katika blog hii
Post a Comment