Unapokwenda katika usaili ni wazi
kwamba unakuwa umejiandaa kujibu maswali kadhaa kutoka kwa mwajiri.Jambo moja
la kuzingatia ni kwamba mwajiri kuna majibu anayotegemea kutoka kwako kwa
kipindi chote cha usaili ambayo ndo hasa msingi wa usaili.Haya ndo majibu
husika soma…
Siku zote
mwajiri jambo la kwanza analotaka kulitambua kutoka kwako ni kuona kama unao
ujuzi wa kazi husika mfano,unaomba nafasi ya afisa masoko.Mwajiri ataangalia
ujuzi ulonao katika nafasi hiyo kulingana na uzoefu mbalimbali.Pia ataangalia
ni maarifa gani utahitaji kupitia mafunzo mbalimbali kazini ili uwe katika
ubora zaidi.
2. Je unaendana na nafasi husika
Kila shirika
linatamani kuona namna gani unaweza kufanyakazi katika idara husika kwa ufanisi
wa hali ya juu.Lakini pia mwajiri anatazama ni kwa vipi unaweza kufanyakazi na
watumishi wenzako na kuwa msaada katika kuwasaidia kuendeleza vipaji vyao
katika kazi.
3. Je unalifahamu shirika na nini
linachofanya?
Kama
shirika linafanya kazi ambazo zinaendana sawa na taaluma yako ni wazi kwamba
utavutiwa kufanya kazi katika shirika hilo.Waajiri wengi wanapenda kusikia
majibu ambayo yanaonesha wazi kuwa wewe hujaomba kazi kwa vile huna kazi au
unataka mshahara ila umeomba kazi kwa vile unapenda kufanya kazi katika shirika
hilo.
4. Je unawezaje kukabiliana na
washindani wenzako?
Unapoenda
katika usaili unalinganishwa na wale ambao pia wameeomba nafasi hiyo,hivyo siku
zote mwajiri anapenda kuona wewe utafanya usaili kwa kiasi gani ili kuweza
kuwashinda wenzio.Hivyo zingatia maandalizi na pia ujue mbinu mbalimbali kwa
kusoma na kutembelea blog mbalimbali ikiwa ni pamoja na blog hii ya Amewezaje.
5. Je unahitaji kazi uloomba?
Waajiri
wengi wanatambua kwamba wale wanaoomba nafasi za kazi ni dhairi wanahitaji kazi
hizo.Utofauti unakuja pale ambapo wengine wanapofanya maandalizi ya kutosha
kuhusu usaili na wengine wanaenda pasipo kuzingatia haya.Jambo la msingi hapa
jitahidi kuthibitisha kuwa unahitaji kazi hiyo kwa kuwa na majibu mazuri ya uhakika.
………..Maktaba YETU leo……….
“If you fulfill the wishes of your employees, the employees will fulfill your visions.”
Amit Kalantri
“If you fulfill the wishes of your employees, the employees will fulfill your visions.”
Amit Kalantri
Post a Comment