What is your greatest strength?
Ni dhairi kwamba suala la ajira katika ulimwengu wa leo ni
la ushindani wa hali ya juu na hivyo kama hautakuwa makini itakuchukua muda
mrefu sana kupata ajira iwe serikalini au katika mashirika au taasisi
zisizokuwa za kiserikali kwani kila mwajiri anataka mtu bora atayeweza
kufanyakazi kwa ufanisi wa hali ya juu.Kipimo muhimu katika hilo ni namna utavyoweza
kujielaza katika usahili.Unaweza kusoma miaka mingi katika taaluma yako lakini
ukashindwa kuelewa kuwa usahili pia ni taaluma.Ukumbuke kuwa hata kuitwa katika
usahili ni jambo la bahati sana sasa, kwa nini usitumie fursa hiyo kupata hiyo
ajira kwa sababu wamekuona unafaa tayari, kilichobaki
ni wewe kwenda kuthibitisha umahiri wako.
Leo nakupatia mbinu thabiti ambazo wengi wamezitumia katika kuijbu
swali hili na kupata ajira bila pingamizi.Kumbuka kwamba wakati wa usahili wale
wanaokusaili(Interviewers) wanakuwa makini sana katika swali hili kuhusu uwezo
wako(your strength) ambapo itaonesha wazi ni jinsi gani unauwezo
katika kazi hiyo.
"What is your greatest strength?"(ni nini uwezo wako) hili ni miongoni mwa maswali rahisi sana
katika interview ingawa wengi wamekuwa wakishindwa kulijibu.Unapoulizwa swali
hili kuhusu uwezo wako jambo kubwa hapa ni kuzingatia sifa ulizonazo ambazo
zitakufanya ufuzu katika nafasi hiyo.
Njia rahisi ni wewe kuelezea ujuzi na uzoefu
ulonao ambao moja kwa moja unaendana na nafasi uloomba.Napozungumzia uzoefu na
ujuzi si maanishi tu kwamba lazima ulikuwa umeajiriwa unawezakuwa umepata
uzoefu na ujuzi hata kutoka shuleni,kujitolea n.k
MAMBO MATATU YA KUZINGATIA.
11. Hakikisha umesoma mchanganuo wa kazi(job description) ili uje nini kinahitajika katika nafasi hiyo.Baadhi
ya matangazo kazi uorodheshe sifa zinazohitajika wakati wengine huwa hawaweki
sifa hizo.Hivyo, unahitaji kukusanya maelezo ya ziada kabla hujaenda katika
usaili. Unaweza kutafuta taarifa kwa, tovuti au kwa mwajiri mwenyewe pale
inapohitajika hii itakusaidia kutambua ni wapi ujikite katika kuelezea uwezo
wako(Strength) kulingana na mahitaji husika.
2 2. Tengeneza orodha maeneo ulio na ujuzi nayo kulingana na hitaji
la nafasi husika.unaweza kuorodhesha sifa
nyingi tu na ujuzi huo wawezakuwa katika elimu,uzoefu wa kazi ,ujuzi
binafsi.Hii itakusaidia kumfanya mwajiri wako atambue kuwa unaujuzi ambao
utasaidia kufanikisha mafanikio ya kazi husika,badala ya kusema tu kuwa
unaujuzi pasipo kutaja ni kwa namna gani umewezapata ujuzi huo.kumbuka kutoa
mifano ni kwa jinsi gani ulitumia ujuzi huo katika kukabiliana na mambo hadi
ukafanikiwa maneno matupu bila mifano katika interview hayana mashiko kabisa.
3. Andaa hadithi fupi.
Njia nyigine ni kuandaa
hadithi ambayo unaeleza namna ulivyotumia uwezo wako katika
kufanikisha tukio Fulani ambalo lilko sawa na nafasi uliyoomba. Matukio haya
lazima lifute utaratibu ambapo unaweza unaweza kuelezea hali au changamoto; na
hatua ulizochukua; na matokeo, uwezo
ulopata au athari za ushiriki wako.lengo
mahususi hapa lazima kuonesha uwezo ulionao ambao unaweza kuutumia pia katika
nafasi unyoomba.
Tazama mifano ya majibu
ya swali hili na imeandikwa kwa lugha ya kiingereza ambapo utaipata kwa ufasaha
zaidi.
“I have
exceeded my sales goals every quarter and I've earned a bonus each year since I started with my
current employer.”
“My
time management skills are excellent and I'm organized, efficient, and take
pride in excelling at my work.”
“I pride myself on my customer service skills
and my ability to resolve what could be difficult situations.”
Post a Comment