Home » » SWALI LITAKALOKUVUSHA KATIKA INTERVIEW,NDO CHANZO CHA MASWALI YOTE..TAZAMA HAPA

SWALI LITAKALOKUVUSHA KATIKA INTERVIEW,NDO CHANZO CHA MASWALI YOTE..TAZAMA HAPA

Written By Unknown on Saturday, August 23, 2014 | 3:27 PM


JE NI JAMBO GANI AMBALO UMEFANIKIWA KULIFANYA KATIKA TAALUMA NA KAZI YAKO MPAKA SASA.. What is the single most significant accomplishment in your career up to this point?
Swali hili ni moja lakini limebeba maswali mengi ambayo yatosha kujibiwa kwa muda wa dakika 30 za usaili na ukijibu vema utapata nafasi unayoomba.,Tazama maswali yake

A.kwanini unafakiri haya ndo mafanikio yako makubwa?
B.Nieleze jinsi ulivyofanya kazi na wenzio na nini yalikuwa majukumu yako
C.Nieleze changamoto 3 ulizokutana nazo na namna ulivyoshughulika nazo
D. Je, unaweza kupima matokeo hayo na kwa nini unafikirii kuwa ni mafanikio?
E.Ukitazama sasa nini ungeweza kufanya cha tofauti na awali na ambacho kingekupa matokeo zaidi ya mwanzo?
F.Kwanini unafikiri ulichaguliwa katika nafasi ile?
G.Kwanini unajisikia fahari kwa mafanikio hayo?
H. Nieleze zaidi kuhusu mienendo ya timu ulofanyanayo kazi na hadi kukamilisha kazi hii
I.Uliwezaje kusimamia mpango wako na hadi kufikia mafanikio?
J.Ni mambo gani uliyapenda katika mradi/shughuli hiyo?
K.Ni mambo gani hukuyapenda  na ni kwa njia zipi ulikabiliana nayo?
L.Uliwezaje kuongozwa,mambo gani uliyapenda na hukuyapenda katika uongozi
M. Eleza baadhi ya makosa makubwa ulofanya, jinsi gani uliyashughulikia , na nini ulijifunza kutokana na makosa hayo?
N. Tafadhali nipe  mifano 5 maalum ya jinsi gani ya ulivyoongoza, na kusimamia  wengine
O.Umejifunza nini kutoka kwa watumishi wenzako
P.Binafsi umewezaje kuongeza uwezo wako kutokana na uzoefu huu?
Q.Ni kwa jinsi gani kutokana na uzoefu ulojifunza utakusaidia katika nafasi hii uloomba leo?
………..Maktaba YETU leo……….
. “Strength does not come from winning. Your struggles develop your strengths. When you go through hardship and decide not to surrender, that is strength”
 Arnold Schwarzenegger


Share this article :

Post a Comment

 
Owner : Amewezaje team | Join us on Facebook | Welcome again
Copyright © 2015. Amewezaje - All Rights Reserved
Designed by Kijiwe Cha Wasomi