Ni dhairi kwamba suala la ajira kwa hivi
sasa ni changamoto kubwa sana,na hivyo pasipokuwa na mbinu mbadala huwezi
kupata ajira kirahisi kwa kipindi kirefu,utafiti unaonesha kuwa wengi wa
wahitimu wanazunguka na bahasha kila uchao pasipo mafanikio na miongoni mwa
sababu kubwa hawana uzoefu wa kutosha.Blog yako ya Amewezaje
inakuletea mbinu rahisi ya kupata kazi,na mbinu hiyo ni kufanya kazi ya
kujitolea Kuna faida nyingi sana katika kufanya kazi ya kujitolea ni wazi kuwa
hata wewe umeshuhudia watu wakipta ajira kwa njia hii.Leo nakupa faida kuu nne
za kufanyakazi kwa kujitolea(Internship/volunteer)
1.
Unapata fursa ya kuandika uzoefu wako katika ‘CV’
yako.Hii itakutengenezea wigo mkubwa wa kupata kazi kwani unaonesha tayari
unafahamu jinsi ya kufanyakazi.
2. Unapata uzoefu unaotakiwa katika
kazi.Waajira mara nyingi wanaangalia uzoefu wa jumla ambao hata wakikuajiri
unawezaanza kazi mara moja.
3.
Kujua kwa undani zaidi kuhusu kazi.Hii ni pamoja
na kupata mbinu mbalimbali za kazi ikiwa ni pamoja na kukabiliana na changamoto
zinapokuwa zinajitokeza katika kazi.
4.Kutengeneza
mtandao na watu mbalimbali.kumbuka kuwa
kufahamiana na watu ni mtaji mkubwa sana katka maisha hivyo ni rahisi sana
kupata kazi.Jitahidi kuwa na mawasiliano ya watu wengi wanaoweza kukupa habari mara
kwa mara.
………..Maktaba YETU leo……….
. “Do not hire a man who
does your work for money, but him who does it for the love of it.”
Henry David Thoreau, Life
without Principle

Post a Comment