Swali,…Kwanini umeacha
kazi ulokuwa unafanya?
Swali hili mara nyingi linakuwa na majibu mbalimbali
lakini inategemea na kazi unayoomba pamoja na mazingira.Blog yako ya Amewezaje
baada ya utafiti kutoka kwa wataalamu mbalimbali wa mambo ya ajira inakuletea
mfululizo wa majibu ambayo unaweza kutumia kujibu swali hili.
a.Nilijiuzulu kwa sababu katika kazi nilokuwa nafanya
kulikuwa hakuna fursa ya kutosha kwa mimi kuendelea katika maneo ya taaluma
yangu.
b.Nilipotoka katika masomo niliamua kutafuta kazi
nyingine kwasababu nilitaka kupata uzoefu tofauti kulingana na taaluma
niloisomea katika chuo.
c.Kusema kweli nafasi nilokuwa nikiitumikia haikuwa
inaendana na taaluma yangu,hivyo nikaona ni vema nijiuzulu katika nafasi hiyo.
d.Kazi nilokuwa nafanya ilikuwa ya muda hivyo nikaamua
kujiuzulu ili nitafute kazi ya mkataba wa muda mrefu.
e.Niliamua kujiuzulu ili niweze kujifunza changamoto mpya
na kujifunza mambo mapya tofauti na nilojifunza katika kazi yangu ya awali.
f.Familia yangu ilibadirisha makazi na kuhamia eneo
jipya na katika eneo hili hakuna ofisi
za shirika nilokuwa nafanya kazi,hivyo niliamua kujiuzulu.
Post a Comment