Mpendwa msomaji siku
zote tunasema kuwa suala la usaili linahitaji umakini wa hali ya juu sana na
hivyo ni vema ukazingatia kila kipengele unachofanya ili kujihakikishia nafasi
unayoomba.Leo blog yako ya Amewezaje inakuonesha makosa ambayo ni madogo
laikini yananafasi kubwa sana katika usaili…
1. Kuchelewa
kufika katika usaili-Hapa itakufanya kutokupata muda wa
kutafakari na kupangilia mambo yako,pia mwajiri atapoteza imani nawewe kuwa
hata wakati utakapoajiriwa waweza kuwa unachelewa maana jambo hili kwako ni la
kawaida(Tabia)
2.
Kutokuzima simu –si rahisi kufahamu ni wakati gani
unawezakupigiwa simu wengi wamepigiwa simu wakiwa katika usaili na matokeo yake
wamepoteza mwelekeo kabisa na hata kukosa nafasi husika.Unaweza kuzima simu au
kuundoa sauti na hata kuweka mtetemo iwapo unaulazima wa kufanya hivyo.Vinginevyo
zima simu ili kuiweka akili yako katika usaili kwa asilimia 100%
3.
Kujibu swali pasipo kulielewa-Wengi hukimbilia kujibu
maswali wakati hawajaelewa na matokeo yake wanajibu isivyosahihi.Siku zote
jitahidi kulielewa swali kama hujaelewa ni vema ukauliza kueleweshwa ili upate
kujibu kwa ufasaha zaidi
4.
Kutokuzigatia lugha ya mwili-Katika usaili lugha ya mwili
ni jambo la msingi sana ambapo ni muhimu kunzigatia.Maelezo zaidi tembelea blog
hii katika matoleo yake ya awali upate kusoma zaidi.
6.
Kuvaa chini zaidi au juu zaidi ya
unavyovaa mara nyingi-Ukivaa chini au juu zaidi
ni dhairi utakuwa katika hali ambayo si ya kawaida na kukufanya muda mwingi
kufikiri juu ya mavazi maana si halisi.Zingatia kuvaa katika kiwango cha
wastani pia zingatia aina ya kazi unayoomba.
7.
Kutokushukuru-Ni vema baada ya usaili ukashukuru kwa njia
utayoona inafaa ingawa njia bora ni kwa barua pepe au barua ya kawaida.Kushukuru
sio mpaka uwe umechaguliwa tu pia kuitwa katika usaili ni jambo la kuwashukuru
kwa kukuona unafaa.
8.
Kusalimia bila kujiamini-Usaili unaanza pale tu unapoonana na
mwajiri wengi wamekuwa na wasiwasi sana wakati wanaposhikana mkono kwa
salamu.Zingatia unaposalimiana na mwajiri toa sauti ya uhakika na umtazame
usoni na kumuuliza jambo moja au mawili.
………..Maktaba YETU leo……….
. “Strength does not come from winning. Your struggles develop your strengths. When you go through hardship and decide not to surrender, that is strength”
. “Strength does not come from winning. Your struggles develop your strengths. When you go through hardship and decide not to surrender, that is strength”
– Arnold
Schwarzenegger
Post a Comment