Ni
utaratibu uliopo mara baada ya kujibu maswali wakati wa usaili (interview)
unapewa fursa kuuliza maswali.Katika
eneo hili ndipo wengi hushindwa kujua ni nini cha kuuliza.Blog yako ya Amewezaje
inakuletea mbinu nyepesi za nini cha kuuliza unapopewa fursa hii. Zingatia
haya:
Hakikisha
unauliza maswali ambayo yataonesha kwa
namna gani utaweza kukizi mahitaji ya mwajiri wako.Mfano unawezauliza mradi
au shughuli mahususi utakazojihusisha nazo pindi watakapokuajiri.Hii itaonesha
jinsi gani unadhamira ya dhati katika kufanya kazi na kuleta tija usiweke maslahi yako mbele
kuliko ya mwajiri.
Unaweza kuhuliza
maswali
kulingana na taarifa zaidi unazofahamu kuhusu shirika hii pia itakuongzea alama
nyingi kwa kuwa utauliza vitu kwa kina zaidi.
Iwapo
hutaambiwa tarehe ya kupata majibu na namna utavyotaarifiwa ni muhimu kuuliza
swali hilo.Wengi husema majibu ni ndani ya siku kadhaa na ukiona hujataarifiwa
ujue hujachaguliwa kama hawajatoa taarifa hiyo ni vizuri ukachukua hatua ya
kufuatilia.Katika mada zinazokuja tutalizungumzia hili kwa kina.
Usiulize
kuhusu mshahara au maslahi mengine kama posho kwa ujumla usiulize mwajiri
atakufanyia nini.Maswali haya yatakuonesha kuwa unatanguliza ubinafisi na sio
kazi kwa ufupi umefuata pesa sio kazi.Si kwamba hupaswi kujua taarifa hizo
lakini pale si mahali sahihi pa kuuliza.Katika mada zetu tutakuonesha ni wapi
pa kuuliza.
………..Maktaba YETU leo……….
. “The key for us, number one, has always been
hiring very smart people.”
– Bill Gates, Microsoft
Post a Comment