Unapokwenda kwenye usaili ni wakati muafaka kwa
mwajiri kuonana nawewe na kupenda kufahamu mambo kadhaa kutoka kwako,kama vile
uwezo wako wa kukabiliana na mamba,utu wako na kwa vipi unaweza kufanya kazi
katika shinikizo(pressure)Kwahiyo ni muda mzuri kwako kuonesha ubora wako
kimasoko na hii itamfanya mwajiri aone sabababu ya kukuajiri.Tatizo kubwa ni
kwamba unakwenda kwenye usaili pasipo kupata habari za taasisi au shirika
husika kwa kufahamu malengo ambapo ndo dira ya shirika hilo.Siku hizi mashirika
mengi yanaweka taarifa zao katika mitandao tafadhali soma kwa kina ili upate
mwanga katika kujibu swali hili.
SWALI:kwanini
unataka tukuajiri?(Why should we hire you?)
Swali
hili mara nyingi huwezi likwepa na wengi wamepoteza nafasi kwa kukosea majibu.Hakuna
kulikosa tena.Zingatia haya mambo manne kwenye majibu yako.unapojibu usiwe na
wasiwasi jibu kwa utulivu na kwa kufurahi.
1.
Tambua ujuzi unaohitajika katika nafasi hiyo(Skills needed for the
job)-Ukieleza usieleze ujuzi nje ya unohitajika….
2. Tambua malengo ya nafasi hiyo(Goals for the
position)-Jieleze ukilenga utafanyanini au unanini kitachochangia malengo hayo
kutimia.
3. Historia yako katika kazi na elimu(Job
background)-Katika hayo maelezo zingatia uzoefu ambao kwa kiasi kikubwa
unashabiliana na kazi unayoomba sio kueleza kila kitu.
4. Zingatia kusoma vizuri mchanganuo wa kazi kwani
huwezi kuoanisha maelezo yako kama hujasoma huo mchanganuo(Job description)
Soma mifano hii kwa maarifa zaidi si kwamba lazima
uitumie kama ilivyo.
Kwanini
unataka tukuajiri?
Katika nafasi hii ya (…JAZA….) katika kampuni hii
kwangu mimi ni nafasi sahihi sana.Nina shahada ya (…JAZA……),nina uzoefu na
maarifa nilivyovipata katika kazi nilokuwa ninifanya katika Kampuni (…TY.).Nina
uwezo mkubwa wa kufanya kazi kwa maadili,na ni mtu wa kutegemewa kaitka kazi
kwani kwa bidii yangu nataraji kufanyakazi kwa kiwango cha juu.
Kwanini
unataka tukuajiri?
Iwapo ninapata fursa hii, ninatajitahidi
kuhakikisha kampuni(XY….) inaongeza
faida na kufikia malengo yake.Nina elimu ya kutosha,ninauwezo wa kufanya kazi
kama kiungo muhimu pia napenda kujifunza vitu mbalimbali katika kazi ili kuleta
ufanisi.Hii nafasi ninaitazamia sana na iwapo nitaipata nitakuwa hazina kubwa
katika shirika hili.
Kwanini
unataka tukuajiri?
"Najisikia kuwa mimi ni mtu sahihi kwa nafasi
hii kwa sababu ya uzoefu wangu, haiba(personalty) yangu, na elimu yangu. Nina
dhamira na ujuzi muhimu kwa ajili ya kazi hii.kumbukumbu za kazi
zitakudhirishia kwamba mimi ni mtu wa kutegemewa, mfanyakazi ngumu , na naweza kufanya
kazi pamoja.Nimevutiwa sana na kampuni hii ya(…CV.. ) na ntajisikia upendeleo
kufanya kazi hapa. "
………..Maktaba
YETU leo……….
“You can’t teach employees
to smile. They have to smile before you hire them.”
Arte
Nathan, Wynn
Las Vegas
+ comments + 1 comments
Uko vizuri kijana, komaa
Post a Comment