Kabla ya kwenda katika usaili ni vema ukakusanya taarifa
za kutosha ambazo zitakusaidia sana
katika kupata nafasi uloomba.Utafiti huu umeganyika katika makundi makuu matatu
kama ifuatavyo
1. Jitafiti wewe mwenyewe(you)-katika
utafiti huu unatakiwa kujiuliza maswali yafuatayo na kupata majibu yake kabla
ya kwenda katika usaili
-Je nina uwezo wa kufanya kazi hiyo?
-Nitawezaje kutimiza malengo ya mwajiri wangu?
2. Fanya utafiti
kuhusu nafasi husika(position)-katika sehemu hii ni vema kuelewa kwa kina nafasi
unayoomba ili kuwa katika mazingira mazuri ya kujibu maswali yanoyoelekezwa
kwenye eneo husika, hakikisha unafahamu haya:-
-Elewa hitaji na majukumu ya nafasi husika
-Zingatia vipengele vyote vya nafasi hiyo na kuvitathimini
kwa kina.
3. Fanya utafiti
kuhusu mwajiri wako pamoja na shirika(Employer & Company)-ni vema
ukafahamu mambo kadhaa kabla ya kwenda katika usaili ili kuwa katika nafasi
nzuri ya kujibu maswali,hivyo ni vema
kuzingatia haya:-
-Historia ya shirika husika
-Shughuli zote zinazofanywa na shirika husika
-Mfumo mzima wa uongozi/utawala wa shirika husika pamoja na
idara zake zote.
Post a Comment