Mpendwa
msomaji mara tu baada ya kumaliza usaili si kwamba utakuwa umekamilisha
majukumu yako yote kwani bado kuna mambo ya msingi unayotakiwa kufanya.Hapa
kuna mambo makuu mawili ya kufanya mara baada ya usaili.
Uliza
kama kuna hatua nyingine ya usaili.Katika usaili kila
taasisi inakuwa na
utaratibu
wake wa kufanya usaili hadi kuajiri,baadhi ya mashirika hufanya usaili kwa njia
tofauti tofauti mfano: Usaili wa kuandika(Written) mahojiano (Oral),kwa njia ya
simu(Phone interview) n.k.Jambo la kuzingatia hapa ni kwamba si taasisi zote
zinaweza kufanya yote kwa wakati mmoja lakini pia zinawezakufanya kwa wakati
mmoja na kurudia ili kufanya mchujo wa kupunguza idadi ya wasailiwa.Hivyo basi
ni vema ukawa na taarifa za kutosha kuhusu hatua za usaili zinazofuata ili
upate muda wa kujiandaa.Unaweza kuuliza pindi tu unapopata fursa ya kuuliza
katika chumba cha usaili ama baada ya usaili.
Tuma
barua ya shukrani.Shukrani ni miongoni mwa mambo ya msingi ambayo mwanadamu
hupenda kutendewa,hivyo hata katika usaili suala hili lina uzito sawa.Ni vema
ukatuma barua fupi yenye sentensi chache za kushukuru kwa fursa na thamani
kubwa ulopewa na taasisi kuitwa katika usaili.Unaweza kuandika barua
pepe(Email)yenye maneno mafupi ya shukrani .Kumbuka ni vema ukaandika barua
ndani ya masaa 24 mara baada ya usaili,kama huwezi kupata fursa ya kuandika
barua mara baada ya usaili unaweza kuandaa na baada ya usaili ukaikabidhi kwa
wahusika.Wengi hawafanyi suala hili
lakini lina nafasi kubwa ingawa baadhi ya taasisi hawalipi suala hili uzito.
Post a Comment