JITAMBUE
Hatua ya kwanza kabla ya kufanya usaili ni
vizuri ukajifanyia tathmini wewe binafsi ili utambue kitu gani unaweza kufanya kwa mwajiri iwapo
utapata fursa.Ni vema ukajitathmini kwa kuzingatia ujuzi na udhoefu ulonao
ambao utakufanya kujiuza zaidi kwa mwajiri wako wakati wote wa usaili.Jambo la
muhimu katika kujiuza kwa mwajiri anza na uzoefu wako katika kazi kwa kutaja na
kuelezea kwa undani shughuli ambazo umekuwa ukizifanya ( Katika ajira ya
awali,Kazi za kujitolea,Miradi shuleni n.k) Kumbuka katika yote hayo usihanisha
na nafasi unayoomba.
ANDAA
MAVAZI UTAKOYOVAA KATIKA USAILI.
Kile utachovaa katika usaili pia ni sehemu
muhimu sana katika maandalizi ya usaili.Ukishatambua nini utavaa katika usaili
siku moja kabla ya usaili ni jambo jema sana kwani utapata fursa ya kujiandaa
katika maeneo mengine ambayo yanahitaji utulivu wa kiakili zaidi.Hivyo
unashauriwa kulifanya suala la mavazi mapema kuliko kusubiri siku ya usaili
laweza kukupotezea muda mwingi sana.
SOMA
WASIFU WAKO (CV) NA KUELEWA KILA KITU
Kila kitu ulichoandika katika “CV” yako
kinaweza kujadiliwa katika usaili,kwa kuwa mwajiri huisoma “CV” yako na
kukufahamu wewe na ndipo hufanya maamuzi ya kukuita katka usaili.Hivyo mwajiri
anaweza kuchagua kipengele kimojawapo katika “CV” yako na kukutaka utoe
ufafanuzi hata kama ni kazi ulofanya kwa kipindi kirefu kilichopita utatakiwa
kukitolea ufafanuzi wa kina.Hivyo zingatia kusoma “CV” yako kwa umakini na
kuelewa kila kipengele katika “CV” yako.
Post a Comment