Wakati wa usaili ni wakati muhimu na hadimu sana,hivyo
unahitaji umakini wa hali ya juu zaidi katika matumizi yake.Baadhi ya maswali
unaweza kuyauliza kumbe ndo inakuwa
safari yako ya kupoteza ajira.Hivyo maswali mengine ni ya kufanya utafiti na
mengine ni ya kumuuliza mwajiri mara baada ya kupata fursa unayoomba.Yafuatayo
si maswali ya kuuliza katika usaili…
1.
Mtanipa mshahara kiasi gani?Swali hili si sahihi wakati
wa usaili sababu kubwa ni kwamba suala la mshahara litakuja mara baada ya
kuchaguliwa katika nafasi husika kutokana na uwezo wako katika usaili.Pia ni
vema ukafanya utafiti kuhusu mshahara mapema ili uje viwango kulingana na
nafasi unayoomba.Kumbuka mara baada ya kupata fursa ndipo mtakapojadili suala
la mshahara nawewe utaona kama kiwango kinafaa.
2.Ni
lini kiwango cha mshahara wangu kitapanda?Hili swali ni baya
pengine kuliko la kwanza.Kuhusu kupanda kwa mshahara inategemea baadhi ya mashirika yako na utaratibu wa wazi lakini
mengine hayako hivyo,jambo la msingi niwewe kufanya utafiti wa kina pindi
unapopata kazi husika.Zingatia kwamba wakati wa usaili wewe unatakiwa kuangalia
suala la kutetea nafasi uloomba sio kuchunguza maslahi.
3.
Je utaratibu wa likizo ukoje katika shirika hili? Swali
hili ukiliuliza ni wazi kwamba uanonesha kuwa hujafanya utafiti wa kutosha
kuhusu shirika,lakini jambo la kuzingatia hapa ni kwamba suala la likizo mara
nyingi ni taarifa ambazo si za siri ni wajibu wako kufuatilia kwa kina kabla
hata hujaomba kazi ili upate kujua wakati mwingine huwekwa hata kwenye mtandao
wa shirika.
………..Maktaba YETU leo……….
Malcolm
Forbes, Forbes
Post a Comment