Home » , » Hizi ndo aina za Usaili(Interview) katika soko la ajira

Hizi ndo aina za Usaili(Interview) katika soko la ajira

Written By Unknown on Friday, January 9, 2015 | 7:07 AM



Kuna aina nyingi tofauti za usaili.Aina hizi utazifahamu mara tu utapochaguliwa katika usaili.Utapochaguliwa katika usaili jitahidi kufanya bidii kujua ni akina nani watashiriki
kukufanyia usaili.Kumbuka kuwa katika usaili ni mara chache sana kufanya usaili wa aina moja  kwani waajiri wengi hupenda kutumia aina nyingi za usaili ili kujiridhisha na aina ya mtu wanayemhitaji.Leo blog yako inakuletea aina mbili za usaili na utaendelea kupata mfululizo wa aina nyingine za usaili.
Usaili wa uso kwa uso(Face to Face Interview)
Katika aina hii ya usaili mara nyingi unaweza kuhusisha  mazungumzo kati ya mtu na mtu .Katika usaili huu jambo la kuzingatia ni kuhakikisha unajikita kwa Yule anayekuuliza maswali kwa kumtazama usoni,kumsikiliza na kujibu maswali pale unapoulizwa.
Lengo kuu kwako ni kuonesha uwezo wako kwa mwajiri na uoneshe ni vipi unaweza kuleta manufaa kwa shirika au taasisi husika.

Usaili wa jopo(Panel Interview)
Katika usaili huu kunakuwa na mtu zaidi ya moja mara nyingi watatu hadi kumi.Huu ndo wakati wako mzuri wa kuonesha uwezo wako wa kuongoza na kuwasilisha katika kwa kundi linalokufanyia usaili.
Kwa kipindi kifupi jitahidi kuhakikisha unasoma na kutambua tabia za kila mmoja na jitahidi kutafuta namna ya kuendana na tabia ya kila mmoja.
Kumbuka kuchukua muda na kuwa makini  katika kujibu maswali.Jitahidi kuwatazama wanajopo pale unapoulizwa swali  na kumtazama anayekuuliza swali.Zingatia matumizi ya lugha ya mwili muda wote unapofafanua hoja.

Endelea kufuatilia aina nyingine za usaili katika blog hii
Share this article :

Post a Comment

 
Owner : Amewezaje team | Join us on Facebook | Welcome again
Copyright © 2015. Amewezaje - All Rights Reserved
Designed by Kijiwe Cha Wasomi