Ni wazi kuwa katika biashara kila kampuni au taasisi huwana
malengo yake ambayo hutaraji kuyafikia katika kipindi fulani.Mara nyingi
malengo hayo hufikiwa kwa kupitia watumishi wa kampuni husika.Baada ya utafiti
wa muda mrefu imegundulika kuwa makampuni ya kibiashara huhitaji watu wenye
sifa kuuu nne.Hivyo unapoandika CV yako zingatia mambo haya ya msingi.
Ni kwa vipi unaweza
kukuza biashara,mfanyabiashara mara zote hupenda kuona biashara yake
ikikuwa,hivyo kama umewahi kufanyakazi kwenye kampuni ya kibiashara na unaomba
kazi onesha ni kwa vipi ulitoa mchango wako katika kukuza biashara ile,Kama
wewe hujawahi kufanya kazi onesha ni kwa vipi unaweza kuchangia katika kukuza
biashara na kampuni kwa ujumla.
Ni kwa vipi unaweza
kutengeneza faida,hakuna biashara isiyohitaji faida ili iweze kujiendesha
Hivyo mwajiri hupenda kuona ni kwa vipi mtumishi anavyoweza kukabiliana na soko
na kuleta faida katika kampuni kwa njia mbalimbali.Hivyo katika CV yako
zingatia sana jambo hilo unapoandika
Ni kwa vipi unaweza
kukuza soko la biashara,Ukuzaji wa
soko mara nyingi umekuwa na tija kwa makampuni kwani huweza kuwafikia wateja
wengi na kuuza bidhaa husika kwa
wingi.Hivyo jambo la kuzingatia kwa mwajiri unapoomba kazi anaangalia udhoefu
wako au mbinu ulizonazo zinazoweza kusaidia katika kukukuza soko.
Ni kwa vipi
unawezakusaidia utengenezaji wa bidhaa mpya.Katika biashara mabadiliko ni
muhimu kutokana na sabababu mbalimbali,hivyo mwajiri yoyote hupenda kuona
mtumishi anayeweza kuleta mabadiliko katika bidhaa,Unapoandika CV zingatia sana
kipengele hiki.
Kumbuka unapoandika CV
onesha mambo ulofanikwa kuyafanya yenyeuhusiano wamoja kwa moja na kazi husika
ondoa mambo yote yasiyo ya lazima katika nafasi husika.
Post a Comment